ndugu nipende kukukaribisha kwenye hii blogu tuweze kujifunza kwa pamoja maswala yahusuyo ualimu ili kuweza kupata maarufa yatakayotusaidia kufanya kazi ya ualimu kwa ufanisi.
katika mazingira ya shuleni ni vema kumpima mwanafunzi wako ili kujua ni kwa kiasi gani anaelewa maarufa unayompatia ili kama hayatoshi uone unavyoweza kuboresha ili ayapate kama yalivyotarajiwa hapa tutakwenda kuonaona maana ya upima katika ngaz ya kielimu
upimaji ni kitendo cha kutaka kujua ni kwa kiasi gani mwanafunzi amepata maarifa yaliyokusudiwa katika somo husika upimaji huu unaweza kufanyika kwa njia mbalimbali ambazo tutakwenda kuziona badae na namna ya kuzitumia
AINA ZA UPIMAJIKatika upimaji wa kielimu tunazo aina kuu nne za upimaji ambazo ni
- upimaji wa awali
- upimaji endelevu
- upimaji tatuzi
- upimaji tamati. Hizi ndizo aina za upimaji wa kielimu ambazo hutumika kumpima.mwanafunzi
Tukianza na ainaa ya kwanza ambayo ni upimaji awali hii ni aina ya upimaji ambayo mwanafunzi hufanyiwa ili kuruhusiwa kuanza ngazi fulani ya elimu mfano mwanafunzi anapoingia au anapoanza darasa la awali huweza kufanyiwa upimaji wa aina hiyo ili kuona kama anaweza kumudu mafunzo ya ngazi hiyo
Hongera Sana
JibuFutaAina zingine za upimaji hazikuelezwa naomba mchango
JibuFuta